Utafiti waonesha vijana wa Kitanzania wanaongoza kwa ustahimilivu wa akili

0
11

Utafiti mpya wa Mental State of the World 2024, uliotolewa na Sapien Labs umebaini vijana wa Kitanzania wana ustahimilivu mkubwa wa kiakili ikilinganishwa na vijana wengine katika nchi 76 zilizofanyiwa utafiti duniani kote.

Kituo cha Utafiti wa Ubongo na Akili cha Sapien Labs kilichopo katika taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Afrika ya Nelson Mandela (NM – AIST) iliyopo jijini Arusha, kimeeleza kuwa kimekusanya takwimu kutoka kwa watu zaidi ya 5,000 kutoka makabila mbalimbali ya Tanzania, jamii na maeneo tofauti ili kuelewa athari za mazingira katika ubongo na akili.

Ripoti hiyo imeeleza kuwa imechambua zaidi ya majibu milioni moja kutoka mtandaoni katika nchi 76 duniani, ambapo matokeo yameonesha Tanzania ni nchi pekee ambayo wastani wa Mental Health Quotient (MHQ) kwa vijana wenye uwezo wa kutumia intaneti unazidi 70.

Aidha, takwimu hiyo imeeleza kuwa takwimu za vijana wa Kitanzania bado ziko chini ikilinganishwa na wastani wa utulivu wa akili wa kundi la watu wazima duniani kote.

Ripoti hiyo imesema sababu zinazosababishwa ustawi wa kiakili kwa vijana wa Kitanzania zinahusisha ulaji wa vyakula vya asili, udhibiti wa mifuko ya plastiki na kiwango kidogo cha sumu itokayo viwandani pamoja na kiwango kidogo cha matumizi ya simu janja wakiwa wadogo, na muda mfupi wanaotumia kwenye simu.

Send this to a friend