Putin akubali kusitisha mapigano nchini Ukraine kwa masharti

0
5

Rais wa Urusi, Vladimir Putin amesema anakubaliana na pendekezo la Marekani la kusitisha mapigano nchini Ukraine kwa siku 30, lakini akisisitiza umuhimu wa kufanyia kazi maelezo yaliyomo katika pendekezo hilo.

Putin pia amependekeza kwamba Ukraine ikomeshe uhamasishaji na mafunzo ya wanajeshi wake, na mataifa mengine yasitishe usambazaji wa silaha kwa Kyiv wakati wa usitishaji mapigano.

Kwa upande wa Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy amemuita Putin mtu mwenye hila na kusema kiongozi huyo anaweza kuchelewesha au kujaribu kuvuruga makubaliano hayo.

Urusi ilivamia Ukraine kwa mara ya kwanza mwaka 2014 na kisha kuanzisha uvamizi kamili mwaka 2022. Wakati huo, Putin alidai Ukraine isiruhusiwe kujiunga na NATO na kwamba muungano huo upunguze uwepo wake wa kijeshi katika Ulaya Mashariki na Kati, madai ambayo Marekani na washirika wake walikataa kwa kuyaita yasiyokubalika, wakilaani uvamizi huo kama unyang’anyi wa ardhi.

Send this to a friend