Marekani yamfukuza Balozi wa Afrika Kusini

0
3

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Marco Rubio, ametangaza kuwa Balozi wa Afrika Kusini nchini Marekani, Ebrahim Rasool, hatakiwi tena nchini humo.

Kupitia mitandao ya kijamii, Rubio amesema Rasool ni mwanasiasa anayechochea ubaguzi na anayeichukia Marekani, huku Rais wa Marekani,  Donald Trump akisema kuwa hawana chochote cha kujadili na yeye.

Hatua hiyo imekuja baada ya Rasool kunukuliwa kwenye moja ya Chombo cha Habari akisema kuwa Trump anaongoza harakati ya kibaguzi dhidi ya viongozi waliopo madarakani nchini Afrika Kusini.

Kulingana na Mkataba wa Vienna wa 1961 kuhusu Mahusiano ya Kidiplomasia, nchi mwenyeji inaweza kumkataa mwanadiplomasia yeyote bila kutoa sababu.

Hata hivyo, uhusiano kati ya Marekani na Afrika Kusini umekuwa ukidorora tangu Trump aingie madarakani.