
Rais wa Urusi, Vladmir Putin ametoa wito kwa wanajeshi wa Ukraine walioko katika eneo la Kursk la Urusi kujisalimisha, huku mazungumzo ya kidiplomasia yakiendelea juu ya uwezekano wa kusitishwa kwa mapigano kati ya Urusi na Ukraine.
Putin amesema ikiwa wanajeshi hao watajisalimisha wataokoa maisha yao pamoja na kupewa matibabu kwa heshima.
Rais Donald Trump amesema wanajeshi hao wamezungukwa na vikosi vya Urusi huku wakiwa katika hali mbaya na hatarini.
Kwa upande mwingine, Putin mempongeza Trump kwa kufanya juhudi kubwa ili kuboresha uhusiano kati ya Urusi na Marekani.