Rais Tinubu atangaza hali ya dharura Jimbo la Rivers, amsimamisha Gavana

0
2

Rais wa Nigeria, Bola Tinubu ametangaza hali ya dharura katika Jimbo la Rivers, linalozalisha mafuta, na kumsimamisha Gavana wa jimbo hilo, Siminalayi Fubara, naibu wake, pamoja na wabunge.

Katika hotuba yake, Tinubu amesema amepokea ripoti za usalama siku mbili zilizopita kuhusu matukio ya uharibifu wa mabomba ya mafuta yaliyofanywa na wanamgambo ambao hawakutajwa bila gavana kuchukua hatua yoyote.

“Hakuna Rais mwenye kuwajibika atakayeangalia tu bila kuchukua hatua. Ili kurejesha utawala bora na amani katika hali hii, imekuwa lazima kutangaza hali ya dharura. Kwa tangazo hili, Gavana Fubara anasimamishwa kazi,” amesema.

Rais Tinubu pia amemtangaza Makamu Admiral Ibok Ete Ibas (Mstaafu) kama Msimamizi pekee wa jimbo hilo kwa muda wa miezi sita ya awali.