Mtambo wa mwisho Bwawa la Mwalimu Nyerere wakamilika

Mtambo wa tisa na wa mwisho katika mradi wa kuzalisha umeme wa Bwawa la Mwalimu Julius Nyerere (JNHPP) tayari umekamilika na kukabidhiwa kwa serikali ikiwa ni hatua ya kuelekea kukamilika kwa mradi huo.
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Doto Biteko amesema serikali imepokea mtambo huo rasmi na upo tayari kuanza kufanya kazi hatua itakayoongeza uzalishaji na upatikanaji wa umeme nchini.
Hayo ameyasema jijini Arusha katika kikao cha Baraza la Kuu la Jumuiya ya Wazazi CCM Taifa ambapo ameeleza kuwa hayo ni moja ya mafanikio makubwa ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan.
Naye Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Fadhili Maganya amesema watafanya kongamano kubwa la kumpongeza Rais Samia Suluhu kwa kutekeleza kikamilifu ilani ya uchaguzi ya CCM katika kipindi cha miaka minne cha uongozi wake.