TAKUKURU yaokoa bilioni 9 mwaka 2024/2025

0
4

Katika kipindi cha kuanzia Julai, 2024 hadi Machi, 2025 Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa (TAKUKURU) imeokoa kiasi cha shilingi bilioni 9.01 na USD 620,000 kutokana na operesheni mbalimbali za uchunguzi zilizofanyika kote nchini.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Nchi – Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene wakati akiwasilisha Makadirio na Matumizi ya Fedha kwa Mwaka 2025/2026, bungeni mkoani Dodoma.

Waziri Simbachawene amesema kati ya fedha hizo, shilingi bilioni 6.01 ni fedha taslimu zilizorejeshwa serikalini na shilingi bilioni 3.00 na USD 620,000 zilidhibitiwa na kurejeshwa katika miradi mbalimbali ya Serikali na kwa walalamikaji wa Sekta binafsi.

Aidha, Waziri ameeleza kuwa katika kipindi hicho, Kesi 867 ziliendeshwa mahakamani zikiwemo kesi mpya 461 ambapo kati ya kesi mpya zilizofunguliwa mahakamani, 10 ni kesi kubwa ambazo zilifunguliwa katika Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, na kesi 451 ziliamuliwa mahakamani.

Ameongeza kuwa katika kesi hizo, Jamhuri ilishinda kesi 352 ikiwa ni asilimia 76.4, ambapo watuhumiwa walihukumiwa kifungo au kulipa faini.

Send this to a friend