Serikali yaongeza mshahara kwa watumishi wa mma na kuhimiza mapitio kwa Sekta Binafsi

0
3

Rais Samia Suluhu Hassan amesema Serikali itaongeza kima cha chini cha mshahara kwa watumishi wa umma kwa asilimia 35.1 kutoka 370,000 hadi 500,000 kuanzia mwezi Julai mwaka huu.

Akizungumza kwenye Maadhimisho ya Sherehe za Siku ya Wafanyakazi (Mei Mosi) ambayo kitaifa yamefanyika mkoani Singida, amesema ngazi nyingine za mshahara pia zitapanda kadiri bajeti ya Serikali itakavyoruhusu.

Amesema kwa upande wa Sekta Binafsi, Bodi ya kima cha chini cha mshaharaa kwa Sekta binafsi inaendelea kufanya mapitio ili kuboresha viwango vya chini vya mshahara kwa Wafanyakazi wa Sekta hiyo.

“Naendelea kuzihimiza wizara na vyama vya wafanyakazi kufanya majadiliano na waajiri ili kutekeleza mikataba ya hali bora ya wafanyakazi katika sekta binafsi waendane sambamba na wenzao wa Sekta ya Umma,” amesema.

Aidha, amewaahidi wafanyakazi kuwa Serikali itaendelea kuboresha mazingira ya kazi yakiwemo maslahi ya wafanyakazi kadiri hali ya uchumi itakavyoruhusu.