Mchungaji akamatwa akiwa na nyoka kwenye begi

0
1

Polisi katika Kaunti ya Busia nchini Kenya wamemkamata mwanaume aliyejulikana kwa jina la Fanish Ramsey Maloba mwenye umri wa miaka 26 baada ya kupatikana na nyoka hai bila kibali kutoka Mamlaka ya Huduma za Wanyamapori Kenya (KWS), karibu na mpaka wa Kenya na Uganda.

Kulingana na ripoti, mwanaume huyo ambaye ni mchungaji wa kanisa la Apostle Ministries Church huko Matayos amekamatwa na maafisa waliokuwa kituo cha polisi cha Mayenje wakati walipokuwa wakilinda eneo la mpakani la Malenya.

Maloba, alipatikana akiwa na begi jeusi lililokuwa na nyoka hai mwenye rangi nyeusi na kahawia mwenye urefu wa takriban mita mbili, alipoulizwa, alidai kuwa nyoka huyo alijitokeza ghafla wakati wa ibada nchini Uganda, na kwamba alimnasa kwa lengo la kumpeleka kanisani kwake kwa ajili ya maombi zaidi.

Baada ya maafisa wa KWS kuwasili pamoja na wapelelezi wa Idara ya Upelelezi (DCI) na polisi kutoka kituo cha Busia, nyoka huyo alikabidhiwa kwa mamlaka ya huduma za wanyamapori.

Send this to a friend