
Mahakama ya Wilaya Kigamboni imemhukumu Paschal Lucas Majandoni (35) kifungo cha miaka 30 jela pamoja na faini ya shilingi milioni moja baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka binti mwenye umri wa miaka 14 mwanafunzi wa darasa la saba.
Upelelezi umeeleza kuwa mshitakiwa huyo alitenda kosa hilo mnamo mwezi Septemba, 2024 maeneo ya Mwongozo Malimbika manispaa ya Kigamboni, Dar es Salaam.
Inaelezwa kuwa mwanaume huyo alimvizia binti akiwa amelala chumbani kwake usiku wakati mzazi wake ameondoka, baada ya kufika alimkuta binti akiwa amelala peke yake chumbani kwake na kufanikiwa kumbaka.
Ushahidi uliowasilishwa Mahakamani hapo umeweza kumtia hatiani Mtuhumiwa na Mahkama kuamuru Mtuhumiwa huyo kutumikia adhabu hiyo ili iwe fundisho kwa wengine.