Rais mstaafu wa Mauritania ahukumiwa miaka 15 jela

0
3

Mahakama ya rufaa nchini Mauritania imemhukumu Rais mstaafu, Mohamed Abdel Aziz kifungo cha miaka 15 jela na faini ya dola milioni 3 baada ya kukata rufaa kupinga kifungo cha miaka mitano.

Aziz alihukumiwa mwaka 2023 baada ya kupatikana na hatia ya utakatishaji fedha ambapo akiwa madarakani, alijipatia mali yenye thamani ya zaidi ya Dola milioni 70 [TZS bilioni 188.8].

Rais huyo mstaafu aliingia madarakani Agosti 06, 2008 hadi Agosti 01, 2019 akihudumu katika nafasi ya urais kwa kipindi cha miaka 11 kabla ya Mohamed Ould Ghazouani kuingia madarakani.

Aziz alisaidia kuongoza mapinduzi mawili kabla ya kuhudumu kwa mihula miwili kama Rais na kuwa mshirika wa kukabiliana na ugaidi katika mataifa ya Magharibi.