
Jeshi la Polisi mkoani Mwanza limesema linamshikilia na linaendelea kumhoji Diana Bundala na maarufu kama Mfalme Zumaridi (42) ambaye ameyageuza makazi yake kuwa kanisa kwa tuhuma za kuendesha shughuli za kidini bila usajili pamoja na kufanya mahubiri kwa sauti ya juu na kusababisha usumbufu.
Taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi imesema Mfalme Zumaridi anahojiwa pia kuhusiana na taarifa inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii ikimuonesha akiwa na kundi la watoto wadogo wa jinsia ta kik3 na kiume, akiwaeleza kuwa yeye ndio Mungu wao mwenye uwezo wa kuwatenganisha na kifo.
“Jeshi la Polisi katika uchunguzi huo litashirikiana na taasisi nyingine za Serikali, hivyo linawaomba wananchi wenye taarifa mbalimbali zinazoweza kusaidia uchunguzi wa tuhuma hizi wafikishe kwa Jeshi la Polisi,” imesema taarifa hiyo.
Jeshi la Polisi limesema uchunguzi utakapokamilika hatua za kisheria zinazostahili zitachukuliwa.