
Mwimbaji wa Nigeria, Simisola Kosoko anayefahamika kwa jina la Simi, amewaomba mashabiki na wananchi waache kumuita binti yake aitwaye Adejare, kwa jina la ‘Duduke’ kwakuwa halina maana yoyote.
Simi alitoa wimbo ulioitwa ‘Duduke’ mwaka 2020, akiwa anasubiri kwa hamu kuzaliwa kwa mtoto wake wa kwanza.
Kutokana na hilo, alipojifungua mtoto wake aliyepewa jina la Adejare pamoja na mumewe ambaye pia ni msanii, Adekunle Gold, baadhi ya mashabiki walianza kumuita mtoto wao kwa jina la “Duduke” kutokana na umaarufu wa wimbo huo.
“Watu wanamuita binti yangu Duduke, jambo ambalo silipendi. Hilo si jina lake. Halina hata maana. Kama lingekuwa na maana nzuri, ningelikubali. Lakini ni mdundo tu, duduke, duduke.
Nilitaka kuonyesha kuwa moyo wangu unapiga kama ngoma. Acheni kumuita mtoto wangu Duduke. Lakini najua inatoka kwenye nia njema, kwa hiyo najaribu kutokukasirika,” amesema.