Nchi 10 maskini zaidi Afrika kwa mwaka 2025

0
233

Bara la Afrika lina karibu asilimia 19 ya watu wote duniani, lakini linachangia chini ya asilimia 3 tu ya uchumi wa dunia wenye jumla ya Dola za Kimarekani trilioni 113.

Kwa mujibu wa makadirio ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) kwa mwaka 2025, Sudan Kusini ndiyo nchi masikini zaidi duniani, ikiwa na pato la taifa kwa kila mtu la Dola za Kimarekani 251 tu kwa mwaka. Hii inaashiria ukubwa wa pengo la umasikini duniani.

Si jambo la kushangaza kuona kuwa nchi nyingi kutoka Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara ndizo zinazoongoza kwenye orodha. Migogoro ya mara kwa mara, taasisi dhaifu, na maendeleo madogo ya viwanda bado ni vikwazo vikubwa vinavyokwamisha ukuaji wa kipato katika eneo hilo.

Kwa mujibu wa IMF, hii ni orodha ya nchi 10 maskini zaidi barani Afrika kulingana na kipato cha kila mtu (GDP) mwaka 2025;

1.        Sudan Kusini: TZS 659,929

2.        Burundi: TZS Milioni 1.29

3.        Jamhuri ya Afrika ya Kati: TZS Milioni 1.4

4.        Malawi: TZS Milioni 1.52

5.        Madagascar: TZS Milioni 1.56

6.        Sudan: TZS 1.64

7.        Msumbuji TZS Milioni 1.74

8.        DRC: TZS Milioni 1.95

9.        Niger: TZS Milioni 1.98

10.      Somalia: TZS Milioni 2.02

Chanzo: Business Insider