Afikishwa mahakamani kwa tuhuma za kumlawiti mtoto wa miaka minne

0
105

Mwanaume anayejulikana kwa jina la Kulwa Steven Ibasa (maarufu kama Baba Claud), mwenye umri wa miaka 37 na mkazi wa Nyakato mkoani Mwanza, amefikishiwa Mahakama ya Wilaya ya Ilemela kwa tuhuma za kumlawiti mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka minne.

Mshtakiwa huyo anadaiwa kutenda kosa hilo Julai 20 na 21, 2025, akiwa nyumbani kwake, ambapo alimuita mtoto huyo sebuleni kwake na kutekeleza kitendo hicho cha kikatili.

Wakili wa Serikali, Mwanahawa Changali ameeleza kuwa mshtakiwa alitumia fursa ya kutokuwepo kwa bibi na mlezi wa mtoto huyo ambaye mara kwa mara huwa anahudhuria ibada kanisani kufanya kitendo hicho.

Hata hivyo, mshtakiwa amekana mashtaka aliyosomewa dhidi yake, ingawa amekiri kumfahamu mtoto husika. Upande wa mashtaka umeeleza kuwa upelelezi wa shauri hilo umekamilika na kuomba mshtakiwa asomewe hoja za awali.

Katika hoja hizo, imebainika kuwa mshtakiwa ni jirani wa bibi wa mtoto huyo, Bi Asteria. Hata hivyo, mshtakiwa amerudishwa mahakamani baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana.

Send this to a friend