Miaka 20 jela kwa kosa la shambulio la aibu kwa mtoto wa miaka minne

0
102

Mahakama ya Wilaya ya Pangani, mkoani Tanga, imemhukumu kifungo cha miaka 20 jela Idd Omary Shelugwaza (26), mkulima na mkazi wa Kijiji cha Kwakibuyu, Kata ya Kipumbwi, Tarafa ya Mwera, wilayani Pangani, baada ya kupatikana na hatia ya kosa la shambulio la aibu dhidi ya mtoto mwenye umri wa miaka minne.

Kosa hilo lilitokea Juni 24, 2025 katika Kijiji cha Kwakibuyu, na baadaye kuripotiwa katika Kituo cha Polisi Pangani, ambako mtuhumiwa alikamatwa na uchunguzi kuanza mara moja.

Wakati wa kusomewa shtaka, mtuhumiwa alikana tuhuma hizo. Hata hivyo, shauri liliendelea kusikilizwa mahakamani ambapo mashahidi mbalimbali walitoa ushahidi, na hatimaye mahakama ikaridhika kuwa ushahidi uliowasilishwa uliuthibitisha kosa hilo bila kuacha shaka.

Send this to a friend