Serikali ya Taliban yapiga marufuku vitabu vilivyoandikwa na wanawake

0
117

Taliban imeondoa vitabu vilivyoandikwa na wanawake kwenye mtaala wa vyuo vikuu nchini Afghanistan, pamoja na kupiga marufuku masomo ya haki za binadamu na unyanyasaji wa kingono.

Takriban vitabu 140 vilivyoandikwa na wanawake vimeingizwa kwenye orodha ya vitabu 680 vinavyokwenda kinyume na Sheria ya Kiislamu na sera za Taliban.

Mmoja wa wanachama wa kamati inayopitia vitabu amethibitisha taarifa hiyo, akiiambia BBC kwamba “vitabu vyote vilivyoandikwa na wanawake haviruhusiwi kufundishwa.”

Serikali ya Taliban imesema inaheshimu haki za wanawake kulingana na tafsiri yao ya tamaduni za Afghanistan na Sheria ya Kiislamu.

Send this to a friend