
Tume Huru ya Uchaguzi nchini Kenya (IEBC) imesema inahitaji KSh bilioni 57.3 [TZS Trilioni 1.09] kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu mwaka 2027, kutoka bajeti ya awali ya KSh. 61.7 bilioni [TZS Trilioni 1.18] iliyopunguzwa na Hazina ya Taifa.
Akizungumza bungeni Alhamisi, Mkurugenzi Mkuu wa IEBC, Marjan Hussein Marjan, amesema kupunguzwa kwa bajeti hiyo kunaweza kuathiri maandalizi ya uchaguzi.
Kamishna Ann Nderitu ameongeza kuwa IEBC inalenga kuandikisha angalau asilimia 70 ya vijana wa Kenya ili kupiga kura huku akieleza kuwa vijana watahamasishwa kupitia mitandaoni.
Aidha, Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria wa IEBC, Chrispine Owiye, amesema tume inatarajia kusajili wapiga kura wapya milioni 6.3 kufikia 2027.







