
Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Kusini, Mtwara imewahukumu kunyongwa hadi kufa mapacha wawili, Daniel Seif (Kurwa) na Daniford Seif (Doto) wenye umri wa miaka 24, wakulima na wakazi wa Kijiji cha Mraushi A, Wilaya ya Masasi mkoani Mtwara, baada ya kupatikana na hatia ya mauaji ya mama yao.
Taarifa ya Polisi imesema watuhumiwa hao walitenda kosa hilo Desemba 15, 2024 kwa kumpiga mama yao mzazi, Upendo Mathew kwenye paji la uso kwa kutumia jembe na mwichi na kumsababishia majeraha yaliyopelekea kifo chake.
Mahakama imeeleza kuwa watuhumiwa hao wote wawili walikiri kutekeleza mauaji hayo ya kikatili baada ya kumtuhumu mama yao kuwa anawaroga.








