
Jeshi la Polisi mkoani Manyara, limesema Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Boay wilayani Babati, Eleth Mtaita hajatekwa isipokuwa anashikiliwa kwa tuhuma za uchochezi.
Mchungaji Mtaita anadaiwa kuhamasisha waumini kutoshiriki uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025.
Akizungumza na Mwananchi, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Manyara, Ahmed Makarani amesema pia wanamtafuta mmoja kati ya masheikhe wa msikiti uliopo eneo hilo la Boay, Juma Silima ambaye anatuhumiwa kuhamasisha watu wasiende kupiga kura.
Amesema viongozi wa dini wanapaswa kujikita katika kuzungumzia masuala ya kumuabudu Mungu na si kujihusisha na mambo ya siasa.







