Rais Samia: Uwaziri Mkuu ni nafasi ya kulitumikia Taifa na wananchi

0
88

Rais Samia Suluhu Hassan amesema nafasi ya Uwaziri Mkuu haihitaji urafiki, undugu na ujamaa, badala yake ni nafasi ya kulitumikia Taifa.

Ameyasema hayo leo Novemba 14, 2025 katika hafla ya kumwapisha Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania iliyofanyika Ikulu Chamwino mkoani Dodoma.

Rais Samia amemwambia Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba kuwa, kwa umri alionao, wadhifa huo ni mzigo mkubwa kwake, kwani atakumbwa na vishawishi vya ndugu, jamaa na marafiki.

“Tukutakie kazi njema, mzigo huu si mdogo na kwa umri wako, sijui Kassim [Majaliwa] aliingia akiwa na umri gani, mzigo huu ni mkubwa, kwa umri wako vishawishi ni vingi vya marafiki, ndugu, jamaa na wengine. Nafasi yako ile haina rafiki, ndugu wala jamaa ni nafasi ya kulitumikia Taifa hili,” amesema.

Aidha, Rais Samia ameongeza kuwa miradi mbalimbali ya kimandeleo imeahidiwa kwa wananchi na muda ni mfinyu, hivyo serikali haina budi kuongeza kasi katika utendaji wake ili kutekeleza yote yaliyoahidiwa.

Send this to a friend