Amuua mume wake kwa kumchoma na chupa ya bia wakiwa klabu

0
75

Polisi katika Kaunti ya Bomet nchini Kenya wamemkamata mwanamke mwenye umri wa miaka 32 akihusishwa na mauaji ya mume wake baada ya mzozo uliotokea katika klabu ya usiku eneo la Kapkwen.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Kaunti hiyo, mtuhumiwa aliyetambulika kwa jina Sharon Cherotich, anadaiwa kuvunja chupa ya bia kisha kutumia ncha yake kali kumchoma shingoni mume wake mwenye umri wa miaka 36, wakati wa ugomvi.

Taarifa za awali zinaeleza kuwa marehemu alipoteza damu nyingi na alifariki dunia akiwa njiani akipelekwa Hospitali ya Tenwek. Sababu ya mzozo huo bado haijabainika.

Aidha, mashahidi wameeleza kuwa wawili hao walikuwa wakinywa pamoja kabla mabishano kugeuka na kuwa vurugu, na baada ya kutekeleza tukio hilo mtuhumiwa alitoroka.

Baada ya uchunguzi wa awali, polisi walimfuatilia na kufanikiwa kumtia mbaroni Cherotich akiwa mafichoni.

Send this to a friend