
Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga linawashilikilia watu watatu wa familia moja kwa tuhuma za mauaji ya mama yao mzazi, Mariamu Ngasa (69), wakimtuhumu kwa uchawi.
Akithibitisha tukio hilo, Kamanda wa Polisi mkoani humo, SACP Janeth Magomi amesema tukio hilo limetokea Desemba 07, mwaka huu majira ya saa 1 jioni, ambapo ameeleza mwili wa Mariamu ulipatikana ukiwa na majeraha makubwa kwenye sehemu mbalimbali za mwili.
“Taarifa za awali zinaonesha kuwa watoto wa mama huyo wanadaiwa kutenda kitendo hicho kutokana na kumtuhumu mama yao kuwa mchawi, amesema Kamanda.
Amesema uchunguzi zaidi unaendelea ili kubaini chanzo kamili cha tukio hilo na kuhakikisha watuhumiwa wanafikishwa mahakamani.







