Serikali yatenga bilioni 11 usajili wa watoto NIDA

0
60

Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imesema inafanya maandalizi ya kusajili watoto wenye umri wa chini ya miaka 18 ili kuwapatia namba ya utambulisho wa kipekee (Jamii Namba) itakayotumika tangu kuzaliwa hadi mwisho wa maisha ya mtu.

Ameyasema hayo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene, katika Kituo cha Kuchakata Taarifa cha Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), wakati wa ziara yake ya kukagua uzalishaji wa vitambulisho.

Ameongeza kuwa zoezi hilo ni utekelezaji wa maelekezo ya Rais Samia Suluhu aliyoyatoa Agosti 10, 2023, na kwamba jumla ya shilingi bilioni 11.3 zimetengwa kwa ajili ya usajili wa watoto.

“Jamii namba itakayowatambua watoto ni jambo kubwa linalokuja. Itapunguza malalamiko mengi kwa sababu mtu atatambulika tangu anapozaliwa,” amesema Waziri Simbachawene.

Naye, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIDA, Omar Mmanga, amesema jumla ya vitambulisho milioni 21.2 vimezalishwa, lengo likiwa ni kuhakikisha kila Mtanzania anakuwa na utambulisho popote alipo.

Send this to a friend