Wananchi watahadharishwa kufuatilia maji wanayotumia kuepuka magonjwa

0
64

Meneja wa Maabara Kuu ya Ubora wa Maji Dar es Salaam, Hashim Kabelwa amewasihi wananchi katika maeneo mbalimbali kuwa makini na kuzingatia usalama wa maji wanayotumia ili kulinda afya zao katika kipindi hiki cha uhaba wa maji.

Hayo yameelezwa katika zoezi la ukaguzi, upimaji na kutibu maji yanayotumika kwa wananchi kupitia visima binafsi na magari binafsi, ambapo amewasihi wananchi kufuatilia na kujua ikiwa chanzo cha maji wanayotumia kimehakikiwa.

“Kutokana na ukame uliopo, kuna watu wasio waaminifu wanaweza kusambaza maji yasiyo salama kiafya na kusababisha mlipuko wa magonjwa, hivyo tunawajibika kukagua miundombinu na kupima usalama wa maji kwa watoa huduma binafsi na kuwahimiza wananchi kuhakikisha wanatambua chanzo cha maji wanayotumia ikiwa kimehakikiwa na Mamlaka ili kuepuka madhara na milipuko inayoweza kujitokeza,” amesema Kabelwa.

Kwa mujibu wa DAWASA, upungufu wa maji Dar es Salaam umesababishwa na kushuka kwa kiwango cha uzalishaji kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kushuka kwa kina cha Mto Ruvu iliyosababishwa na kuchelewa kwa mvua.

Send this to a friend