Polisi kuchunguzwa kuhusu vifo vitatu vya watuhumiwa

0
36

Jeshi la Polisi limesema linamshikilia Askari Polisi Mkoa wa Kipolisi Rufiji kwa tuhuma za kumpiga risasi Shaban Said Luluba, Mkazi wa Kijiji cha Nyamwage na kupelekea kufariki.

Taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi imesema tukio hilo limetokea leo wakati wa ukamataji ambapo Polisi wamesema endapo itabainika kuna uzembe au matumizi zaidi ya nguvu hatua nyingine za kisheria zitachukuliwa dhidi ya askari huyo.

Katika hatua nyingine, Jeshi la Polisi limesema linachunguza kifo cha Dickson Thaddeus Joseph, mkazi wa Rebu Senta wilayani Tarime mkoani Mara baada ya kupokea malalamiko kuwa kifo chake hakikutokana na kuanguka wakati akikimbia katika Mtaa wa Serengeti, bali kimesababishwa na askari polisi.

Aidha, Jeshi la Polisi limesema linachunguza tukio lingine ni la Viollete Uwumuhoza, Raia wa Rwanda ambaye alijinyonga Januari 7, 2026 akiwa mahabusu ya Polisi Jijini Arusha, alikokuwa akishiliwa kwa kosa la kuingia na kuishi nchini kinyume cha Sheria.

Send this to a friend