
Katibu Mkuu wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), Salum Mwalimu amepata ajali usiku wa kuamkia Januari 20, 2026, katika eneo la Morocco, Dar es Salaam.
Polisi wamesema ajali hiyo imetokea baada ya gari aina ya Subaru Forester kugonga kwa nyuma gari aina ya Toyota Prado lililokuwa likiendeshwa na Mwalimu kisha kupoteza mwelekeo na kuingia katika eneo la kuuza magari, ambapo liligonga magari mengine matatu.
Aidha, polisi wameeleza kuwa majeruhi wa ajali hiyo, Moza Ally tayari amepatiwa matibabu na kuruhusiwa, na dereva wa Subaru Paschal Emmanuel, mkazi wa Goba Dar es Salaam anashikiliwa na polisi.







