Mama ashikiliwa tuhuma za kuua watoto wake watatu wakiwemo pacha

0
33

Polisi wa Mlolongo, Kaunti ya Machakos nchini Kenya wanamshikilia mwanamke aitwaye Linet Mubaba, anayedaiwa kuwapa sumu watoto wake watatu baada ya kutokea ugomvi wa kifamilia kati yake na mume wake.

Mwanamke huyo, amekamatwa siku ya Jumanne baada ya miili ya watoto wake watatu wakiwemo pacha wa kike wa mwaka mmoja na mtoto mmoja wa kiume wa miaka minne kupatikana nyumbani kwao.

Taarifa za awali zinaeleza kuwa tukio hilo lilitokea baada ya kutokuelewana kati ya Mubaba na mume wake, Alex Mogeni, ambaye ni dereva. Polisi wanasema inadaiwa kuwa Mubaba alikimbia eneo la tukio, lakini baadaye alifuatiliwa na kukamatwa.

Miili ya watoto hao imehifadhiwa kwa ajili ya uchunguzi wa kitabibu ili kubaini chanzo halisi cha vifo vyao.

Send this to a friend