
Serikali ya kijeshi ya Burkina Faso imetoa amri ya kufuta vyama vyote vya siasa, ambapo tayari vilikuwa vimesitisha shughuli zake tangu mapinduzi ya kijeshi, na kwamba mali za vyama zitachukuliwa na serikali.
Waziri wa mambo ya ndani amesema uamuzi huo ni sehemu ya juhudi za kujenga upya nchi, kwani wingi wa vyama vya siasa ulisababisha migawanyiko na kudhoofisha mshikamano wa jamii.
Kabla ya mapinduzi, Burkina Faso ilikuwa na zaidi ya vyama 100 vya siasa, huku 15 vikiwa na uwakilishi bungeni baada ya uchaguzi wa mwaka 2020.







