
Kampuni 408 za Tanzania zimepata usajili wa Mamlaka Kuu ya Forodha ya Jamhuri ya Watu wa China (GACC) jambo linaloziruhusu kusafirisha mazao ya kilimo kwenda soko la China.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA), Prof. Joseph Ndunguru, amesema usajili wa kampuni hizo utaongeza thamani ya mazao ya kilimo, kuimarisha biashara nje ya nchi na kuchochea ukuaji wa uchumi.
Ameongeza kuwa kampuni lazima zizingatie viwango vya afya ya mimea, matumizi sahihi ya viuatilifu na ukaguzi unaohitajika kabla ya kusafirisha bidhaa.
Prof. Ndunguru pia amewataka wafanyabiashara na wakulima kufuata sheria na kanuni ili Tanzania iweze kufaidika kikamilifu na fursa za soko la China.







