Fainali Klabu Bingwa ilivyozua mzozo CAF hadi CAS

0
0

Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limetangaza Morocco kuwa bingwa wa AFCON 2025, miezi miwili baada ya michuano kumalizika. Senegal amepokonywa ubingwa huo kwa kukiuka kanuni, ambapo Morocco imepewa ushindi wa magoli 3-0 hatua iliyozua mijadala mingi sehemu mbalimbali duniani.

Si mara ya kwanza CAF kufanya uamuzi unaozua mjadala. Mnamo Mei 2019, katika mechi ya marudiano ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Espérance de Tunis na Wydad Casablanca, mwamuzi kutoka Gambia, Bakary Gassama, alitangaza Espérance kuwa mabingwa baada ya wachezaji wa Wydad kuondoka uwanjani kufuatia uamuzi wa mwamuzi wa kukataa bao la kipindi cha pili la Walid El Karti.

Kwa mchezo uliosimama kwa zaidi ya saa moja na upande wa Wydad kukataa kuendelea kucheza, Gassama alimaliza mechi na kuipa timu ya Tunisia ushindi wa 3-0, jambo lililosababisha fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kusitishwa ikiwa ni mara ya kwanza katika historia yake.

Ingawa uamuzi wa Gassama ulikuwa unaendana na kanuni za mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na sheria za mchezo, kamati ya utendaji ya CAF ilikutana Paris mwezi Juni na kuupindua uamuzi huo, ikiamuru mechi hiyo ya marudiano ichezwe upya.

Hatimaye, uamuzi huo ulilazimika kuheshimiwa baada ya Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS) kuingilia kati, na kuthibitisha Espérance kama mabingwa.

Send this to a friend