Abiria kutoka Tanzania wakamatwa India na dhahabu ya wizi 53kg

0
56

Kilo 61 za dhahabu zenye thamani ya Rand 320 milioni (TZS bilioni 9.18) zimenaswa katika visa viwili tofauti katika uwanja wa ndege nchini India huku abiria saba wakishikiliwa na Polisi wakiwemo Wahindi wanne kutoka Tanzania.

Katika kisa cha kwanza, maofisa wa forodha wamewakamata Wahindi wanne waliotua kutoka Tanzania wakiwa wamebeba dhahabu ya magendo kilo 53 huku wengine watatu akiwemo bibi wa miaka 61 aliyekuwa kwenye kiti cha magurudumu akitokea Dubai wakikamatwa na kilo 8 za dhahabu.

Precision Air yaanza taratibu za kuwalipa waathirika wa ajali

Kwa mujibu wa ripoti kutoka chombo cha habari cha The Indian Express wakati wa mahojiano na abiria hao, wote wanne wamekiri kuwa walikabidhiwa dhahabu hizo wakiwa katika usafiri wa anga katika uwanja wa ndege wa Doha na raia asiyejulikana wa Sudan ambaye hakuwa amesafiri nao kwenye ndege.

Idara ya forodha katika Uwanja wa Ndege wa Mumbai imesema kiwango kilichokamatwa ni kiasi kikubwa kuwahi kukamatwa, na kwamba wote waliokamatwa wamerejeshwa rumande kwa siku 14 na mahakama ya Hakimu Mkazi.

Send this to a friend