Abiria sasa kuingia Stendi ya Magufuli kwa kadi za kulipia

0
41

Manispaa ya Ubungo imeanzisha utaratibu mpya wa kuingia katika Stendi Kuu ya Mabasi ya Magufuli kwa kutumia kadi (N-Card), ili kuboresha huduma za usafiri na usafirishaji pamoja na kudhibiti upotevu wa mapato kwa abiria wanaoingia katika kituo hicho.

Akizungumza na Swahili Times, Kaimu Ofisa Habari wa Manispaa ya Ubungo, Joina Nzali amesema kituo hicho kinachohudumia watu wengi ndani na nje ya nchi, ni ngumu kukusanya mapato hasa wakati wa asubuhi kutokana na mrundikano wa watu kuwa mkubwa.

“Tumeona ni vyema sasa tukaja na mfumo ambao utakuwa ni rahisi kwa watu wote, hakuna anayeumizwa wala anayependelewa. Serikali itakusanya mapato na mwananchi atapata huduma katika hali ya haraka na ubora zaidi,” amesema.

Jeshi la Polisi lasema halina utani

Aidha, amesema hata kwa wale wasindikizaji pia watahitajika kuwa na kadi hiyo ambazo zipo za aina mbili moja ikiwa TZS 300 inayotumika mara moja tu na nyingine ni TZS 1000 ambayo inaweza kutumika katika huduma zingine kama, kulipia kivuko na kadhalika.

Halikadhalika amesema kwa abiria asiyekuwa na kadi akifika stendi atapatiwa kadi ya kutumia mara moja ambayo akipita itabaki kwenye mlango kwa kumezwa na kukusanywa kama ushuru getini hapo.

Send this to a friend