Achapwa hadi kufariki kwa kuaibisha familia kwa ulevi

0
50

Leshoo Mollel (90) na wanawe watatu Simon Leshoo (35), Baraka Leshoo (38) na Abedi Leshoo (15), wakazi wa Kijiji cha Munge wilayani Siha mkoani Kilimanjaro wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za mauaji ya ndugu yao wakimtuhumu kushiriki kikao cha usuluhishi akiwa amelewa.

Taarifa kutoka eneo la tukio zinaeleza watuhumiwa hao wanadaiwa kumwadhibu ndugu yao kwa kumchapa kwa fimbo sehemu mbalimbali za mwili, huku wakimtuhumu kuwaaibisha kwa kushiriki kikao cha usuluhishi akiwa amelewa kitendo kilichowakera ndugu hao.

Kijana akamatwa kwa tuhuma za kuiba mtoto tangu mwaka 2020

Akizungumzia tukio hilo, Mwenyekiti wa Kijiji cha Munge, Isack Mollel amesema tukio hilo limetokea Oktoba 24, 2022 na alipata taarifa kutoka kwa balozi wa eneo hilo, kuwa kijana huyo amefariki baada ya kuchapwa fimbo sehemu mbalimbali.

“Tukio hili limetokana na masuala ya kifamilia. Familia ilimchapa fimbo hadi kufariki, walikuwa wakimuadhibu kutokana na tatizo la ulevi. Walimfunga kamba wakamchapa fimbo akafariki dunia,” amedai.

Send this to a friend