ACT Wazalendo waitaka Serikali imhoji Balozi kilichotokea Angola

0
3

Chama cha ACT Wazalendo kimeitaka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kufafanua kilichotokea nchini Angola na kutia msimamo wa Serikali juu ya suala hilo.

Tamko hilo limekuja baada ya viongozi wa vyama mbalimbali kuzuiliwa kuingia nchini Luanda kwa ajili ya kushiriki mkutano kuhusu masuala ya demokrasia akiwemo kiongozi wa chama hicho, Dorothy Semu, Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, ambaye pia ni Mwenyekiti wa ACT Wazalendo, Othman Masoud na wengine.

Aidha, Chama hicho kimeitaka Serikali kumuita mara moja Balozi wa Angola nchini Tanzania kujielezea kilichotokea kwa viongozi hao.

Hata hivyo, viongozi wa ACT Wazalendo waliozuiliwa nchini humo tayari wamerejea nchini.

Mazungumzo ya Jukwaa la Demokrasia Afrika The Platform for African Democrats (PAD) yaliandaliwa na Taasisi ya The Brenthurst Foundation

Send this to a friend