ACT Wazalendo wamtaka Jaji Mkuu na Jaji Biswalo wajiuzulu

0
40

Chama cha ACT-Wazalendo kimemtaka Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Juma na aliyekuwa Mkurugenzi wa Mashtaka ambaye sasa ni Jaji wa Mahakama Kuu, Biswalo Mganga wajiuzulu nafasi zao ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazowakabili.

Uamuzi huo umekuja baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kueleza kuhusu upotevu wa fedha zilizopatikana kutoka kwa watu waliokuwa wakikabiliwa na kesi mbalimbali kupitia utaratibu wa ‘plea bargaining.’

Taarifa ya Rais Samia imepigilia misumari taarifa iliyotolewa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) katika ripoti yake ya Aprili 2021 ambapo ilionesha mabilioni ya fedha yaliyokusanywa hayajulikani yalipo.

Kanisa Katoliki laishtaki CCM na Serikali kwa madai ya kupora ardhi

Katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na kiongozi wa chama hicho, Zitto Kabwe ameeleza kuwa Jaji Mkuu na Jaji Biswalo wanapaswa kujiuzulu nafasi zao kwa kuwa madai ya kupotea kwa fedha za ‘plea bargaining’ yalitokea wakati wao wakiwa wasimamizi.

“ACT-Wazalendo inataka ufanyike uchunguzi huru na wa haraka ili kufichua ukweli wote nyuma ya utaratibu wa plea bargaining. Watakaothibitika kuhusuika na upotevu wa mabilioni wachukuliwa hatua,” kimeeleza chama hicho huku kikisisitiza kuwa watu na taasisi zisizo na hatia ambazo zilipoteza fedha kwenye mkakati huo, zipatiwe haki zao.

Send this to a friend