ACT Wazalendo wamtaka Waziri Mchengerwa kuwarejesha wagombea wao waliokatwa

0
34

Chama cha ACT Wazalendo kimemtaka Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mohamed Mchengerwa kuwarejesha wagombea wote wa chama hicho ambao wamekatwa katika mchakato wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

Katika taarifa iliyotolewa na ACT Wazalendo, imesema chama hicho kimetoa maelekezo kwa wagombea walioenguliwa kukata rufaa kwa mujibu wa kanuni na mwongozo wa uchaguzi didi ya maamuzi yaliyofanywa na wasimamizi wa uchaguzi nchini.

“Ni muhimu kwa TAMISEMI kuhakikisha kuwa wagombea wanatendewa haki ili kila mgombea mwenye sifa apate nafasi ya kugombea na kuchaguliwa kwa misingi ya kanuni,” imeeleza.

Hapo jana, Waziri Mchengerwa aliwataka wagombea wote ambao hawajaridhishwa na uteuzi wa wagombea wa nafasi mbalimbali kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa waweke pingamizi ndani ya siku mbili kuanzia Novemba 08 hadi 09, 2024.

Send this to a friend