ACT Wazalendo yamteua Membe kuwa Mshauri Mkuu

0
41

Chama cha upinzani nchini Tanzania, ACT Wazalendo kimemteua Bernard Membe kuwa Mshauri Mkuu wa chama hicho.

Taarifa iliyotolewa na kiongozi wa chama, Zitto Kabwe imeeleza kuwa uteuzi huo umeanza Agosti 2, 2020.

Aidha, Kabwe amesema kuwa kiongozi huyo mpya atatekeleza majukumu yake kama yalivyoainishwa kwenye katiba ya chama.

Membe ambaye ni mgombea wa urais wa Tanzania kupitia chama hicho, alipokelewa rasmi ndani ha chama hicho wiki chache zilizopita baada ya kufukuzwa uanachama wa Chama cha Mapinduzi.

Mwanasiasa huyo amewahi kushika nyadhifa mbalimbali serikalini, ambapo hadi mwaka 2015 alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania.

Send this to a friend