ACT-Wazalendo yataka mabadiliko ya mfumo wa uchaguzi Zanzibar

0
50

Chama cha ACT-Wazalendo kimetaka kufanyika mabadiliko ya mfumo wa uchaguzi Zanzibar ili kurejesha imani ya wananchi juu ya uwepo wa uchaguzi huru na wa haki.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa ACT-Wazalendo, Ado Shaibu leo jijini Dar es Salaam wakati akitangaza maamuzi ya Kamati Kuu ya chama hicho iliyokutana jana jijini Dar es Salaam Disemba 5, 2020.

Maazimio memgine ya kikao hicho ni chama hicho kuridhia kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) Zanzbar na kiwaruhusu wawakilishi, wabunge na madiwani waliochaguliwa katika uchaguzi wa Oktoba 28, 2020 kuendelea na majukumu yao.

https://twitter.com/ACTwazalendo/status/1335516232125038593?s=20

Chama hicho kimesema kuwa sababu ya kukubali kuunda serikali ni kutokana na hali ya Zanzibar ambapo siasa za chuki na uhasama zimerudi upya na kwamba inahitajika busara kubwa katika kuponya majeraha yaliyotokana na uchaguzi.

Aidha, Shaibu amesema chama hicho kimetaka kufanyika uchunguzi wa matukio ya ukiukwaji wa haki za binadamu kabla, wakati na baada ya uchaguzi na wahusika wachukiliwe hatua na walioathiriwa wanafarijiwe.

Maalim Seif Sharif Hamad alipeperusha bendera ya chama hicho visiwani Zanzibar ambapo alishika nafasi ya pili baada ya kupata kura asilimia 19.87 ya kura zote halali.

Send this to a friend