ACT yataka Dkt. Slaa na wenzake wapelekwa mahakamani au waachiwe huru

0
39

Chama cha ACT Wazalendo kimelitaka Jeshi la Polisi kuwaachia huru bila masharti yoyote au kuwapeleka mahakamani Wakili Boniphace Mabukusu, Mpaluka Nyagali na Balozi Dkt. Wilibroad Slaa.

Katika taarifa iliyotolewa na chama hicho leo, imepinga kitendo cha polisi kukaa na watuhumiwa hao kwa zaidi ya saa 48 kinyume na sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai kifungu cha 32 kinachowataka polisi kumfikisha mtuhumiwa mahakamani au kumwachia huru ndani ya muda huo.

“Wakili Boniphace Mwabukusu na wenzake wapo kwenye mikono ya Jeshi la Polisi tangu 11 Agosti, 2023 bila kupelekwa mahakamani,” imeeleza taarifa.

Polisi wathibitisha kuwashikilia Mwabukusi na Mdude, msako unaendelea

Aidha, chama hicho kimetaka mageuzi ya Jeshi la Polisi katika kuimarisha mfumo wa haki jinai na kuondoa changamoto nyingi ambazo chama kimedai zinapelekea uonevu, ukandamizaji, unyanyasaji na ukiukwaji wa haki za binadamu.

Send this to a friend