Adai kukatwa mkono na mumewe baada ya kuchelewa kurudi nyumbani

0
6

Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga linamtafuta Charles Peter mkazi wa Kata ya Mwendakulima, Manispaa ya Kahama mkoani humo kwa tuhuma za kumkata mkono wa kushoto mke wake, Hapiness Khalfan (30) baada ya kutokea ugomvi.

Kamanda wa Polisi mkoani humo, Janeth Magomi amesema baada ya mwanamke huyo kuhojiwa amedai kuwa chanzo cha kufanya ukatili huo ni baada ya mwanamke huyo kuchelewa kurudi nyumbani na kwamba Jeshi la Polisi linaendelea kufanya uchunguzi zaidi.

Aidha, imeelezwa kuwa baada ya tukio hilo, mwanamke huyo hakutoa taarifa mahali popote, ila baadhi ya majirani waliripoti polisi, ambapo polisi wanaendelea kumtafu mtuhumiwa ambaye alitoroka.

Hali ya mwanamke huyo kwa sasa inaendelea vizuri baada ya kupokea matibabu katika kituo cha afya cha Mwendakulima.