Adaiwa kumchinja mkewe mjamzito, kutoa watoto tumboni na kumpika mmoja

0
39

Jeshi la Polisi mkoani Tabora linamshikilia Hamis Kulwa (35), mkazi wa Kata ya Uyogo wilayani Urambo kwa tuhuma za kumchinja mke wake mjamzito, kumpasua tumbo kisha kutoa watoto pacha.

Akizungumza Kamanda wa Polisi mkoani humo, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Richard Abwao amesema tukio hilo limefanyika Januari 30 mwaka huu saa 11 jioni likihusishwa na imani za kishirikina.

Kamanda Abwa amesema baada ya mtuhumiwa kumpasua mke wake, alitoa watoto pacha kisha kumpika mmoja huku mwingine pamoja na mwanaye mwingine aliyekuwa na miaka miwili, akiwazika.

Zanzibar yapiga marufuku wamasai kutembea na silaha

“Wakati wa mahojiano alidai kuwa aliambiwa kuna watu wametumwa kumchukua mkewe na watoto, wanawapeleka Gambushi [eneo lililoko mkoani Simiyu linaloamika kwa nguvu za giza] kufanya kazi za kichawi usiku na siku si nyingi wangewachukua na kuwaua, ndio maana akaamua awaue yeye mwenyewe,” amesema Kamanda.

Jeshi la Polisi limesema linaendelea na upelelezi na mara ukikamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani.

Send this to a friend