Adaiwa kumuua mama yake wakigombea mali za baba yake

0
46

Jeshi la Polisi limesema mwanamke aliyefahamika kwa jina la Adela Dominick (74) ameuawa kwa kupigwa na kitu butu kichwani kisha kunyongwa kwa kutumia kipande cha kanga na mtoto wake aitwaye Nemes Dominic maeneo ya Uru Okaseni, wilayani Moshi mkoani Kilimanjaro.

Akithibitisha tukio hilo Kamanda Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa amesema chanzo cha mauaji hayo kinachunguzwa lakini wawili hao walikuwa na ugomvi wa muda mrefu wakigombea mashamba na mali za marehemu.

Inadaiwa kuwa mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 54 alifanya tukio hilo usiku wa Septemba 23, 2024 na kisha kutelekeza mwili wa mama yake ndani ya chumba chake alichokuwa anaishi ambapo mwili huo ulikutwa ukiwa umelazwa kifudifudi huku shingoni kukiwa kumefungwa kipande cha kanga.

Kamanda Maigwa amesema jeshi hilo linamshikilia mwanaume huyo kwa ajili ya mahojiano zaidi.

Send this to a friend