Adaiwa kumuua mwanae mlemavu kwa kushindwa kumtunza

0
38

Jeshi la Polisi mkoani Geita linamshikilia mtu mmoja aliyetambulika kwa jina la Elias Bakumye (32) mkazi wa Kijiji cha Chikobe, Kata ya Butundwe wilaya ya Geita mkoani humo kwa tuhuma za kumuua mwanae mlemavu wa viungo na kumzika porini.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Jeshi la Polisi, Kamishina Msaidizi wa Polisi Safia Jongo amesema mtoto huyo alikuwa na umri wa miaka mitano na mwili wake uliokotwa na wasamalia wema Aprili 12 majira ya saa tatu asubuhi.

Jongo amesema baada ya kupokea taarifa hizo walituma timu ya upelelezi kwenda eneo la tukio ambapo baada ya kufika eneo la tukio walikuta mwili ambapo ulionekana marehemu alikuwa ni mlemavu.

Mwanafunzi atolewa korodani baada ya kupigwa na walimu wake

“Alikaa na mtoto akaona hawezi kuendelea kumuhudumia yule mtoto akaamua kumbeba yule mtoto kumpeleka kwa mama yake ambaye alivyofika kule wazazi pamoja na yule mwanamke, mtalaka wake, wakakataa kumpokea yule mtoto alipofika eneo la porini hapo anakiri kwamba akaona yeye hataweza kumuuguza huyu mtoto kwa hiyo akambana pumzi na kumuua na hatimaye akamfukia,” amesema Kamanda Jongo.

Kamanda Jongo amesema mwili huo ulikutwa umeshambuliwa na wanyama na kuonekana kupata michubuko.

Send this to a friend