Adaiwa kumuua mwenzake wakigombea maji ya kupika ili ‘kulegeza’ Swaumu

0
43

Jeshi la Polisi linamshikilia, Hassan Nyundo kwa tuhuma za kumchoma kisu na kusababisha kifo cha Amiri Mohamed (24) mkazi wa Kijiji cha Vuo, Wilaya ya Mkinga wakati wakigombania maji ya kupikia.

Mauaji hayo yamefanyika Aprili 05, 2023 saa 4 asubuhi kwa mujibu wa habari zilizopatikana na kuthibitishwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga, Henry Mwaibambe.

Mashuhuda wa tukio hilo wamedai vijana hao waumini wa dini ya Kiislamu hujificha kwa siri ili kupika na kula wakati huu wa mfungo, hivyo mchana huenda katika kibanda kilichojificha ili kupika kwa tahadhari ya kuonekana na waliofunga Ramadhani.

“Hakane Nyundo alimfuata mwenzake Amiri na kumtaka ampe maji yaliyokuwa kwenye ndoo ili apikie, lakini Amiri alipokataa, wakashikana. Alipoona anazidiwa nguvu akaenda kuchukua kisu na kumchoma,” amesema Husna Hamad.

Polisi: Madereva watembee na vyeti vya udereva, tutavikagua

Aidha, Mwenyekiti wa Serikali ya Kitongoji, Mohamed Kunema amesema baada ya kuchomwa kisu kwenye ubavu wa kushoto, uongozi ulimuwahisha Kituo cha Afya cha Kiwengu ambako waliamua kumpa rufaa ya kwenda Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga ya Bombo lakini alifariki alipokuwa njiani.

“Hawa vijana hawana kawaida ya kufunga mwezi Mtukufu wa Ramadhani huamua kwenda kwenye mageto kujipikia na kula mchana kwa kificho…Sijui ilikuwaje Nyundo alipoona amezidiwa akaamua kumchoma kisu mwezie,” amesema Mwenyekiti.

Send this to a friend