Adaiwa kuua mtoto ili kulipiza kisasi kwa mama yake

0
40

Polisi Mkoani Njombe wanamshikilia Hapiness Mkolwe (27) kwa tuhuma za kumuua mtoto Jackson Kiungo (6) mwanafunzi wa darasa la kwanza katika Shule ya msingi Ihanga kwa madai ya kulipiza kisasi kwa mama wa mtoto huyo aliyekuwa akinywa pombe na mume wake baada ya kutengana.

Kamanda wa Polisi mkoani humo, Hamisi Issah amethibitisha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo ambapo amesema siku ya tukio mwanafunzi huyo alikwenda saluni kunyoa, lakini katika hali isiyo ya kawaida mtuhumiwa alimfuata na kumsubiri kisha kuondoka naye kusikojulikana.

Ameeleza kuwa baada ya kufika huko mtuhumiwa alimsababishia kifo Jackson na kumvua nguo kisha kumfukia kwenye kaburi alilolichimba mwenyewe.

Kamanda amesema kisa kilichosababisha mauaji hayo, kwa mujibu wa maelezo ya mwanamke huyo ni kuwa wametengana na mume wake na kuna mwanamke mwingine ambaye ni mama wa mtoto huyo ambaye alikuwa anakunywa pombe na mumewe, hivyo alipopewa taarifa na watu wake aliamua kulipa kisasi.

Hata hivyo, mtuhumiwa amekamatwa baada ya Polisi kupata taarifa ya kupotea kwa mwanafunzi Septemba 6, mwaka huu.

Chanzo: Nipashe