Mwanaume mmoja kutoka Australia ambaye alijifanya ametekwa nyara ili kuwa na muda na mpenzi wake wa kando siku ya mwaka mpya ameamriwa kulipa gharama za operesheni ya polisi iliyofanyika kumtafuta.
Paul Lera (35) alifika katika mahakama ya Wollongong huko New South Wales siku ya Jumanne na akapewa agizo la kulipa kiasi cha takriban dola 10,000 [TZS milioni 25] kwa saa 200 ya kazi ya polisi yaliyotumika baada ya mwenza wake kuripoti kutoweka kwake.
Mwanaume huyo alikwenda kukutana na mpenzi wake wa kando Desemba 31, lakini alimwambia mke wake kwamba alikuwa anakutana na mshauri wake wa kifedha.
Inaeleza kuwa wawili hao walimtumia mke wake ujumbe wa simu uliosomeka kama ametakwa nyara lakini ujumbe huo ulisambaa na kusababisha hofu zaidi na ndipo mpenzi wake aliporipoti polisi na kuanza kufanya msako.
Lera na mpenzi wake wa kando walizuiliwa asubuhi iliyofuata lakini hata hivyo alidai kuwa alikuwa amechukuliwa na kundi la wanaume wasiojulikana ambao baadaye walimwacha aende zake ingawa baadaye alikamatwa kwa kutoa shtaka la uongo.