Adanganywa na mganga afanye mauaji ili aongezewe nguvu za kiume

0
85

Mkazi wa Kijiji cha Matandarani Wilaya ya Mpanda mkoani Katavi, Joseph Adolf maarufu kama Kisubi, amehukumiwa adhabu ya kifo baada ya kushirikiana na mganga wa kienyeji kumuua Juma Shemeli baada ya kuahidiwa kupewa dawa za kuongeza nguvu za kiume.

Mganga huyo aliyejulikana kwa jina la Joseph Petro ambaye Polisi hawakufanikiwa kumkamata, alimuomba Kisubi ambaye walikuwa maswahiba washirikiane kumuua Shemeli ili achukue nyumba na mali za marehemu.

Inaelezwa mauaji hayo yalitokea Septemba 2, 2020 katika Kijiji cha Matandarani na baada ya mauaji hayo, Kisubi walishirikiana na Petro kuuzika mwili wa marehemu katika shimo la choo nyumbani kwa Petro.

Hukumu hiyo imetolewa Agosti 19, 2024 na Jaji Thadeo Mwenempazi baada ya kusikiliza ushahidi wa mashtaka na utetezi wa mshtakiwa na kujiridhisha kuwa mtuhumiwa alitekeleza tukio hilo.

Katika maelezo yake, Kisubi alikiri kuhadaiwa na Petro kuwa wakifanikiwa kumuua Shemeli, angempatia dawa hiyo kwa kuwa uume wake ulikuwa hausimami wakati wa kufanya tendo la ndoa.

Send this to a friend