Afa maji akijipiga selfie kwenye maporomoko

0
54

Athuman Rashid mkazi wa Balan’ga Wilaya ya Kilindi mkoani Tanga amefariki wakati akijipiga picha (selfie) katika eneo lililokuwa likipokea maji yaliyokuwa yakiporomoka kutoka milimani.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Kamishna Msaidizi (ACP), Henry Mwaibambe amesema marehemu alipatwa na mkasa huo mwishoni mwa wiki akiwa katika Kata ya Kisangasa.

RC Makalla: Mgao wa maji Dar umeisha

Akisimulia tukio hilo Kamanda Mwaibambe ameeleza kuwa marehemu Athuman alisombwa na maji yaliyokuwa yakiporomoka kutoka milimani kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.

“Inaelezwa kuwa maji hayo yalikuwa yakielekea Mto Balan’ga yaliwavutia wanachi wengi kusogea karibu kushangaa maji hayo na ndipo marehemu alipoamua kuyakanyanga ili kujipiga picha na ndipo maji hayo yalipomzidi nguvu na kumzamisha,” amesema.

Send this to a friend