Afande Rama aachiwa huru, Jamhuri yashindwa kutoa uthibitisho

0
44

Mahakama ya Mkoa wa Vuga mjini Unguja imemwachia huru mshtakiwa Ramadhan Ali maarufu kama Afande Rama aliyekuwa akikabiliwa na mashtaka ya kuingiliwa kinyume na maumbile.

Afande Rama ameachiwa huru baada ya hakimu wa mahakama hiyo, Khamis Simai kudai kuwa mshtakiwa hana hatia chini ya kifungu cha 220 ya sheria namba 7 ya mwaka 2018.

Kesi hiyo namba 59 ya mwaka 2023 ilianza kusikilizwa mahakamani hapo ambapo jumla ya mashahidi tisa kutoka upande wa mwendesha mashtaka waliwasilisha ushahidi wao ambao hawakuweza kumtia hatiani mtuhumiwa.

Ramadhani ambaye ni mtumishi wa Jeshi la Polisi, alishtakiwa baada ya kusambaa kwa video katika mitandao ya kijamii zilizodhaniwa kuwa ni yeye ambaye alionekana akishiriki tendo la kuingiliwa kinyume na maumbile.

Send this to a friend